M-KOPA ni Kampuni ya kimataifa inayotoa huduma za nishati kwa wateja walio nje ya Gridi ya Taifa kwa mtindo wa kulipia kidogo kidogo., Kampuni imekuwa ikiendelea pamoja na kufanya majaribio kwa kipindi cha miaka 2 , M-KOPA alianza mauzo ya kibiashara nchini Kenya mwezi wa kumi mwaka 2012. Na kupanua wigo shughuli zake nchini Uganda mwaka 2013 na Tanzania mwishoni mwa 2014.
Mpaka kufikia mwezi wa tisa 2014, Kampuni imeweza kutoa umeme wa Nishati ya Jua kwa garama nafuu kwenye zaidi ya kaya 100,000 na kuongeza zaidi ya kaya 2,500 kila wiki. Kampuni ina wafanyakazi Zaidi ya 400 wanaouza Bidhaa kwa wauzaji wa dogo na wamawakala Zaidi ya 1000
Waasisi wa Kampuni ni wabunifu wazoefu wa Teknolojia ya simu za viganjani wenye uwezo na Imani ya kuleta mabadiliko endelevu ya kitekinologia zaidi , bidhaa nafuu kwa watumiaji iliyoundwa kwaajili ya kunufaisha wateja
Maendeleo hupatikana kwa kuchanganya teknologia bora na juhuhudi endelevu katika Nyanja zote ili kufikia malengo , kwa upande mwingine M-KOPA imeruhusu leseni ya Teknolojia yake kutumika na washika dau wengine kwenye masoko ya nje ya Africa Mashariki (kwa maelezo kuhusu zaidi leseni yatumwe licensing@m-kopa.com )